Friday, August 24, 2012

JESHI LA POLISI KUWACHUKULIA HATUA KALI WATAKAO HUJUMU ZOEZI LA SENSA


Kamishna Paul Chagonja
JESHI la Polisi nchini kuwachulia hatua kali kwa watu ambao watahujumu zoezi la sensa ya Watu na Makazi inayotarajiwa kuanza Agasti 26 mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Oparesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Kamishna Paul Chagonja alisema jeshi limejipanga katika kuhakikisha zoezi la sensa linafanyika katika hali utulivu pasipokuwepo na uvunjifu wa amani wa kutaka kuhujumu zoezi hilo.
Chagonja alisema kuwa watu ambao watafanya uhalifu ikiwemo kuchana karatasi za makarani wa sensa watachuliwa hatua kwa kuwafikisha mahakamani kutokana na sheria ya sensa.
Alisema kuwa kususia sensa ni kosa ambapo aliwataka wenye malalamiko kutekeleza zoezi katika hali usalama na baadaye baada ya kazi hiyo kukamilika ndio wafuatilie madai yao.
“Jeshi halitaweza kuwaacha watu ambao wanataka kuhujumu zoezi la sensa ambalo liko kisheria kwa madai yao wanatumia taasisi katika kushawishi wananchi wasijitokeze katika zoezi ambalo watendaji wetu wametekeleza hadi kufikia hapo”.alisema Chagonja.
Kwa Upande wa Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai Robert Manumba alisema kuwa tayari jeshi la polisi linawashikilia watu kutokana na kutaka kuhujumu zoezi hilo.
Alisema bado wanaendelea kufuatilia kwa karibu juu ya watu ambao wanashawishi wananchi kugoma katika kuhesabiwa kwa sababu zao ambazo haziko kisheria.
Manumba aliwataka wananchi kushirikiana kwa kutoa taarifa za watu ambao wanaopita kwa kubandika sitika katika nyumba juu ya kugomea sensa.
CHANZO; http://francisdande.blogspot.com



Love to hear what you think!