Vurugu Za Zanzibar
J
eshi
la Polisi Zanzibar limelazimika kutumia Mabomu ya Machozi ili
kuwatawanya wafuasi wa kikundi cha Uamsho waliokuwa wamekusanyika
kufanya Dua ya kuwaombea watu waliokufa katika ajali ya kuzama kwa Meli
ya Mv. Skagit katika Mitaa ya Mbuyuni.
Habari kutoka Zanzibar zinadai kuwa Jeshi hilo la Polisi
lililazimika kutumia Mabomu ya Machozi kutokana na kikundi hicho cha
Uamsho kuanza kuhubiri siasa badala ya kufanya Dua hatua iliyosabaisha
kuvunjika kwa amani katika mitaa hiyo.
Mwandishi wa Kituo hiki cha Uhuru FM aliyeko Mjini Zanzibar
amesema licha ya Watanzania kuendelea kuomboleza vifo vya watu
waliokufa katika ajali hiyo, bado kikundi hicho cha Uamusho kimeendelea
kufanya sisasa badala ya kufanya Dua.
Pia
imeelezwa kuwa chanzo cha Mabomu hayo ya Machozi ni kikundi hicho
kufanya Dua yenye utata huku masuala ya siasa yakijitokeza hatua
iliyopelekea kuwepo kwa vurugu za hapa na pale hivyo Jeshi likaamua
kutumia nguvu ya ziada ili kuwatawanya.
CHANZO: Radio Uhuru FM