NI NYUMBA, KUTA ZA MABILIONI ZILIZOJENGWA UFUKWENI, MMOJA AKIMBILIA KORTINI KUZUIA JUMBA LAKE LA SH1.5 BILIONI
SERIKALI jana ilikunjua makucha yake kwa vigogo waliojenga nyumba za
kifahari kando ya Mito ya Mbezi Beach, Mndumbwe na eneo la Hifadhi ya
Mikoko, Dar es Salaam baada ya kuzibomoa katika operesheni iliyosimamiwa
na Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) cha Jeshi la Polisi.
Hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa tamko la Makamu wa Rais la mwaka 2004 ambalo lilitaja maeneo tengefu ambayo yalipaswa kuhifadhiwa zikiwamo fukwe za bahari ambazo zina mikoko ambayo ni mazalia ya samaki baharini. Licha ya tamko hilo na sheria mbalimbali, bado maeneo ya fukwe za bahari yamekuwa yakivamiwa.
Katika kusimamia sheria na tamko hilo, Wizara ya Maliasili na Utalii, Kitengo cha Hifadhi ya Misitu, Baraza la Taifa la Kuhifadhi Mazingira (NEMC) na Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, ziliamua kuratibu bomoabomoa hiyo ya nyumba za kifahari zilizojengwa maeneo tengefu ya bahari.
Bomoabomoa hiyo ambayo iliendeshwa chini ya ulinzi mkali wa polisi wa FFU chini ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela na kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Uzingatiaji na Utekelezaji wa NEMC, Dk Robert Ntakamulenga, jumla ya nyumba 27 kati ya hizo 15 zikiwa zimekamilika ujenzi, nane uzio (fence) na nyingine katika hatua za awali za ujenzi, zilibomolewa.
Kazi ya kubomoa nyumba hizo iliyofanywa na kampuni ya Majembe Auction Mart, ilianza huku wakazi wa nyumba hizo wakiwekwa chini ya ulinzi mkali wa FFU na polisi wengine waliokuwa wamesheheni mabomu ya machozi, bunduki na gari la kumwaga maji ya kuwasha.
Bomoabomoa hiyo ilianzia katika eneo la Hifadhi ya Mikoko, Mbezi Beach mnamo saa 2:00 asubuhi na watu waliokuwa wakiishi katika nyumba hizo walilazimika kutoa vitu vyao nje huku kububujikwa machozi.
Mmoja wa wakazi wa eneo hilo na Mchungaji wa Kanisa la Dar es Salaam Christian, George Makala alisema kitendo hicho kinasikitisha kwa kuwa muda uliotolewa kwao ni mdogo na wasingeweza kujiandaa kuhama.

Akizungumzia shughuli hiyo ya jana, Kaimu Mkurugenzi Usimamizi
Rasilimali na Wakala wa Huduma za Misitu, Zawadi Mbwambo alisema kazi
hiyo imechelewa kutokana na kuhusisha idara, wizara na taasisi tofauti
katika utendaji wake.
Alisema kazi hiyo itakuwa endelevu na itawahusu watu wote waliojenga katika maeneo ya fukwe za bahari na kusisitiza kuwa umbali unaoruhusiwa kujenga nyumba kutoka eneo la bahari ni meta 60.
Kwa upande wake, Dk Ntakamulenga alisema kazi hiyo ya kubomoa nyumba katika maeneo ya hifadhi za taifa, fukwe za bahari na kando ya mito ni endelevu na akatoa wito kwa watu wote waliojenga katika maeneo hayo kuchukuka tahadhari mapema kuondoa usumbufu.
“Tumechelewa kuchukua hatua kutokana na zoezi hili kushirikisha mamlaka zaidi ya mmoja, tulikutana kujadili na kuona umuhimu wa kuunganisha nguvu ili utekelezaji wake usiingilie mamlaka nyingine,” alisema Dk Ntakamulenga.
Alisema kazi hiyo pindi itakapomalizika katika jiji la Dar es Salaam ambako kuna viwanja zaidi ya 100, vinavyopaswa kurudishwa katika mamlaka husika, itahamia mikoani na itawahusu pia watu wote waliojenga nyumba zao kwenye hifadhi za taifa, kando ya mito na kwenye fukwe za bahari kitendo kinachosababisha uharibifu wa mazingira.
Polisi Kinondoni yatoa onyo
Kamanda Kenyela aliwataka watu wote waliojenga nyumba zao katika maeneo yanayokatazwa na Serikali, kuzibomoa wenyewe ili kukwepa mkono wa sheria.
“Tukio la leo ni kwamba tumewasha taa, sasa watu wote waliojenga nyumba zao kinyume na sheria katika jiji la Dar es Salaam na hata wenye migogoro ya ardhi ambao Mahakama ilishatoa hukumu ni vyema wakabomoa wenyewe, watii sheria pasipo shuruti,” alisema.