Tuesday, July 24, 2012

MKUTANO WA CHADEMA WILAYANI SIMANJIRO JANA CHADEMA WAFUNIKA


SAM_2955    Godbless Lema akiunguruma jukwaani hapo jana.
SAM_2779 Ally Bananga aliewahi kuwa mjumbe wa kamati kuu CCM akiwakilisha vijana Arusha kabla ya kuhamia Chadema akiongea na wananchi wa Mirerani kupitia vipaza sauti vya gari la matangazo wakati msafara ukielekea uwanjani kuanza mkutano wa mwisho hapo jana.…
SAM_2755 Chopa inayotumiwa na CHADEMA ikijiandaa kupaa kutoka viwanja vya NMC Arusha kuelekea Simanjiro. Ndani yake wakiwemo Mh Godbless Lema, Alphonce Mawazo na James Ole Millya.
SAM_2955   Godbless Lema akiunguruma jukwaani hapo jana.
SAM_2779 Ally Bananga aliewahi kuwa mjumbe wa kamati kuu CCM akiwakilisha vijana Arusha kabla ya kuhamia Chadema akiongea na wananchi wa Mirerani kupitia vipaza sauti vya gari la matangazo wakati msafara ukielekea uwanjani kuanza mkutano wa mwisho hapo jana.
SAM_2870 James Millya akizungumza na wananchi wa Mirerani.
SAM_2974SAM_2936
SAM_2974Sehemu ya wananchi waliohudhuria mkutano huo.
----
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeendelea na operesheni yake ya M4C kuzunguka maeneo mbalimbali ya nchi kujua mizizi ya matatizo mbalimbali yanayowakabili Watanzania nchini kote, na kukiweka chama karibu zaidi na wananchi.

Safari hii ilikuwa ni zamu ya wakazi wa Wilaya ya Simanjiro, Mkoani Manyara kutembelewa na makamanda wa chama hicho hapo jana wakiongozwa na Mjumbe wa Kamati Kuu wa chama, Mh Godbless Lema.

Mh Lema aliambatana na viongozi na makamanda wengine wakiwemo wanachama wapya waliohamia chama hicho hivi karibuni kutokea CCM. Miongoni mwao ni pamoja na James Ole Millya, Ally Bananga na Alphonce Mawazo.

Jumla ya mikutano saba ilifanyika kwa siku ya jana, sita ikifanyika kwa kuzuru maeneo tofauti ya Simanjiro kwa kutumia helcopta na baadae kumalizia na mkutano mkubwa wa jioni katika uwanja wa shule ya msingi Mirerani iliyopo eneo la Mirerani. Lema, Mawazo na Millya ndio waliotumia chopa na wengine walitumia gari mpya za chama hicho kwa njia za barabara kutokea Arusha Mjini.





Love to hear what you think!