Meneja wa bendi hiyo, Khamis Mujibu, akizungumza jambo mbele ya waandishi wa habari ).
Meza kuu kutoka kushoto ni Mujibu, Ally Choki na kiongozi wa bendi, Rogate Hega ‘Katapila’ wakiwa katika hafla hiyo.
Choki (katikati) akifafanua jambo.…
Meneja wa bendi hiyo, Khamis Mujibu, akizungumza jambo mbele ya waandishi wa habari
Meza kuu kutoka kushoto ni Mujibu, Ally Choki na kiongozi wa bendi, Rogate Hega ‘Katapila’ wakiwa katika hafla hiyo.
Choki (katikati) akifafanua jambo.
Akisoma majina ya wanamuziki watakaosafiri.
BENDI ya Extra Bongo ‘Wazee wa Kizigo’ inayomilikiwa na Ally Choki imepata shavu la kufanya shoo mwezi mzima nchini Finland.Akizungumza na waandishi wa habari ndani ya ukumbi wao mpya wa New White House uliopo Kimara jijini Dar es Salaam, Ally Choki, amesema wanatarajia kuondoka nchini Jumamosi usiku ambapo wataondoka watu 15 wakiwa ni wanamuziki, wacheza shoo na wapiga vyombo ambao ni Rogate Ega ‘Katapila’, Otilia Boniface, Musa Hassan ‘Super Nyamwela’, Isaack Buruani ‘Danger Boy’, Angela Joshua, Lightness, Martin Kibosho, Hosea Muhoji, Adam Hassan, Tom Nhigula, Salum Issa ‘Chakuku’, Athanas Michael, Emmanuel Michael ‘Bob Kisa’, Ramadhan Muhoza ‘Pentagon’ na mdhamini wa bendi hiyo, Chief Kiumbe.
PICHA: GLADNESS MALLYA, GPL