Tuesday, August 21, 2012

BI KIDUDE (FATMA BINTI BARAKA) ANA HALI MBAYA

 



Taarifa kutoka Zanzibar zinadai kuwa mwanamuziki mkongwe wa Taarab nchini Bi. Kidude anaumwa na hana msaada wowote.
Inadaiwa kuwa mjukuu wake alizungumza na televisheni ya Zanzibar na kulalamika kuwa bibi yake hana msaada na hivyo kumuuguza kwa shida.
Taarifa zaidi zinasema Bi. Kidude anaumwa tangu wiki iliyopita.na hana mdau hata mmoja wa muziki aliyejitokeza kumsaidia hivyo natoa wito kwa wadau wenye uwezo wajitokeze kumsaidia bi kidude ili apate matibabu na arejee katika hali yake ya kawaida






Love to hear what you think!