Saturday, December 27, 2014

Bibi Kizee Akutwa Kaanguka Nje Ya Kanisa Asubuni Alipokuwa Akiwanga Usiku


Bibi kizee mmoja huko mkoani Mbeya ambae jina lake halikuweza kufaamika mara moja, amekutwa ameanguka nje ya kanisa akiwa uchi wa mnyama kwa kile kilichodaiwa alikuwa anawanga.
Kikongwe huyo alionekana ni mwenye kuishiwa nguvu pia kuhema sana, alipozinduka alijikuta amezingirwa na watu asubuhi huku akiwa ni mwenye woga wa wingi wa watu hao. Katika kumuhoji haraka haraka alieleza kuwa alikuwa anasafiri safari zake za usiku kutokea mkoani Morogoro kuelekea Ruvuma na alipopita maeneo hayo ya kanisa alijikuta anavutwa na kitu asichokijua ndipo kukapelekea kuanguka kwake.
Watu wa maeneo ya bibi huyo alipoanguka hawakuweza kumtambua na kuonekana hakuwa anaishi hapo ndipo walipomuuliza anakotoka na akajibu kuwa anatokea mkoani Morogoro na alikuwa anaenda Ruvuma kikazi yaani kazi zake za kishirikina.
Tukio la wachawi kuanguka karibu na maeneo ya makanisa mkoa wa Mbeya hutokea mara kwa mara na hivi inajiidhirisha kuwa nguvu za giza zinazotawala maeneo mbalimbali mbele ya mungu hufifishwa kama yaliyomkuta kikongwe huyu.Love to hear what you think!