Thursday, September 12, 2013

ALIYEFUMANIWA NA KICHANGA APEWA TALAKA TATU


Na Issa Mnally
MWANAMKE Rukia Issa maarufu kama mama Sabrina ambaye wiki iliyopita alifumaniwa na mumewe akiwa gesti na mwanaume mwingine huku akiwa na kichanga cha miezi miwili ameachwa kwa talaka tatu.
Mama Sabrina akijifunga khanga baada ya fumanizi.
Akizungumza kwa njia ya simu akiwa nyumbani kwake Goba, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam mume wa Rukia, Shukuru Nia amesema kuwa baada ya kumfumania mkewe akiwa na mtoto wao mchanga na kijana aitwaye Ally Said walienda Polisi Oysterbay ambako walitakiwa kwenda kulimaliza suala hilo katika Serikali ya Mtaa ya Goba wanapoishi wote watatu.
“Katika kikao hicho cha serikali ya mtaa iliamuliwa Ally anilipe fidia ya shilingi milioni mbili lakini akaomba ajikusanye anitafutie milioni moja ambazo atanilipa kidogokidogo nikamkubalia,” alisema mume huyo.
Shukuru ameongeza kuwa baada ya kumalizika kwa kikao hicho alimkabidhi mkewe ambaye amebahatika kuzaa naye watoto watatu talaka tatu ili kuvunja ndoa yao na kutoa ruhusa kuolewa na Bwana Ally.
...Akimbeba mwanaye.
“Kitendo cha mke wangu  kwenda na mtoto mchanga gesti kufanya mapenzi na mwanaume mwingine hakiwezi kuvumiliwa na mwanaume yeyote hapa duniani,” alisema Shukuru kwa uchungu.
Aidha, Shukuru alisema anapatwa na wasiwasi kuhusu mtoto wao huyo aliyezaa na mwanamke huyo kama ni wa kwake au la, hivyo ameamua kumwachia mtoto huyo bwana Ally.
Hivi karibuni Shukuru alimfumania mkewe akiwa gesti maeneo ya Mbagala jijini Dar huku mtoto wao mchanga akiwa amelazwa pembeni ya kitanda wakati wawili hao walipokuwa wakifanya vitu vyao.
Rukia alimuaga mumewe anakwenda Kongowe msibani usiku aliondoka kwenda gesti alikopanga kukutana na Ally.


Love to hear what you think!