Saturday, August 24, 2013

MFANYABIASHARA AKWAA SKENDO MBAYA!

Stori: Mwandishi wetu, Moshi
CD zinazomuonesha mfanyabiashara mmoja mjini Moshi akifanya ngono zinauzwa kama njugu mjini hapa, Risasi Jumamosi limegundua.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa CD hizo zimekuwa zikiuzwa kwa wingi maeneo ya stendi ya mabasi ambapo awali moja bei yake ni shilingi kati ya 4,000 na 5,000 lakini sasa zimepanda na kufikia shilingi 50,000 kutokana na watu wengi kuhitaji.
Sehemu nyingine ambayo mwandishi wetu alibaini kuuzwa CD hizo za ngono ni sokoni pamoja na kwenye viwanja vya mpira ambako vijana wamekuwa wakichangamkia kununua.
Video hiyo inadaiwa kuibwa na mtu asiyejulikana kutoka kwenye kompyuta mpakato (Laptop) ya mfanyabaishara huyo na haijajulikana ni nani aliyeingia katika kompyuta hiyo na kunakili picha hizo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, ACP Robert Boaz, amesema mtuhumiwa wa sakata hilo la CD ya ngono ni  kijana mmoja ambaye anamiliki maduka ya kuuza na kutengeneza CD katika kituo kikuu cha mabasi cha mjini Moshi na tayari amekamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), akitokea Dubai.
“Tulikuwa tunafanya uchunguzi wa picha zilizosambaa kwenye mitandao pamoja na simu kwenye whatsapp ambazo zinaonyesha watu wakifanya mapenzi kinyume cha maumbile, kimsingi ni kosa la jinai mwanamke kumruhusu mwanaume amuingilie kinyume cha maumbile ama mwanaume amuingilie kinyume na maumbile,” alisema Kamanda Boaz.
  Aliongeza kuwa bado uchunguzi wa picha hizo unaendelea ikiwa ni pamoja na kumhoji mhusika na kwamba endapo uchunguzi utakamilika atafikishwa mahakamani kwa kosa la kushiriki kufanya mapenzi kinyume cha maumbile kinyume na kifungu namba 154 cha kanuni ya adhabu; kimeweka adhabu ya kifungo cha maisha kwa mtu anayepatikana na hatia ya kufanya mapenzi na mtu mwingine kinyume cha maumbile.
Inadaiwa kuwa mfanyabiashara huyo kijana alirekodi video hizo kwa siri bila mfanyakazi wake huyo kujua na kuihifadhi kwenye kompyuta ambazo moja kati ya vipande hivyo inaonyesha akimlawiti mfanyakazi wake huyo.
  Katika hatua nyingine, taarifa mbalimbali kutoka eneo la stendi kuu ya mabasi zinasema baadhi ya wasichana wanaodaiwa kufanya mapenzi na kijana huyo wameingiwa na hofu kutokana na kuwa na wasiwasi kuwa huwenda kuna video nyingine ambazo zinadaiwa kurekodiwa na kijana huyo akifanya mapenzi nao.
  “Hapa stendi sasa hivi mabinti waliotembea na jamaa wako roho juu maana wamekuwa na wasiwasi kuwa inawezekana mshikaji aliwarekodi kila msichana aliyetembea naye, sasa wana hofu kwani alichofanyiwa mwenzao kimewatia mashaka,” alisema kijana mmoja muuzaji wa duka la CD ambaye hakupenda jina lake kutajwa gazetini
.Love to hear what you think!