Tuesday, February 26, 2013

kijiji cha ufuska.


Na Mwandishi Wetu
SIKU  chache baada ya gazeti la Ijumaa kuibua danguro la vigogo maeneo ya Kinondoni jijini Dar es Salaam na wahusika kutiwa mbaroni na polisi, mwishoni mwa wiki waandishi  wamekifumua kijiji cha ufuska.
Kijiji hicho kilichogunduliwa Mbagala Zakhem, jijini Dar, wasichana na wavulana walinaswa wakifanya vitendo vya ngono kwenye moja ya mabanda ambayo yametengenezwa maalumu kwa shughuli hiyo.
Awali, waandishi wetu walipata taarifa kutoka kwa wasamaria za kuwepo kijiji hicho pembezoni mwa barabara ya kwenda Kiburugwa, hivyo kuamua kufuatilia.
Operesheni hiyo ilifanywa na waandishi  kwa kushirikiana na jeshi la polisi Jumamosi iliyopita usiku ambapo ilifanikiwa kuwanasa baadhi ya vijana akiwemo mwanamke mmoja aliyekutwa akifanya ngono na wanaume wawili (walio pichani).
Hata hivyo, kundi la watu kama wanane wakiwa na nguo mikononi walitimua mbio baada ya kuona polisi wamevamia chumba kimoja kilichotengenezwa kwa uzio wa vipande vya magunia chakavu na makaratasi walichokuwa wakikitumia kufanyia ngono.
Aidha, wana usalama walifanikiwa kuwakamata watu watatu, wanaume wawili pamoja na mwanamke aliyejitambulisha kwa jina moja la Semeni waliyekuwa wakifanya naye mapenzi.
Baada ya kuwatia mbaroni watu hao na kuwafanyia upekuzi, walikutwa na kondomo na vipisi vya bangi.
Maafande walipomhoji Semeni alisema vijana hao walimlipa shilingi 5,000 kila mmoja na mmiliki wa eneo hilo aliyemtaja kwa jina moja la Babu walimlipa shilingi 2,000.
Mtu mmoja aliyeshuhudia tukio hilo, aliwapongeza polisi kwa kufanikiwa kuwakamata baadhi ya vijana hao.
“Kwa kweli sehemu hii ni kama kijiji cha ngono maana hata wanafunzi huchukuliwa  na kuingizwa kwenye vibanda hivi kwa ajili ya kufanya ufuska, tunashukuru kwa kuamua kukisambatisha,” alisema jamaa huyo aliyeomba hifadhi ya jina lake.

Love to hear what you think!